​ELIMU YA VITABU SI UFUNGUO WA MAISHA

Bottomline: Ukiwadadisi kwa undani wakwasi waliofanikiwa kimaisha, utakuta ya kwamba ufunguo wa mafanikio yao si elimu ya vitabu bali ni elimu ya maisha. 

__________________________________
Mwandishi Ramadhan Sigomba

Tafakari! Kipofu anatoka mastakimuni mwake akielekea mkahawani aidha kupiga gumzo ama kubugia sharubati. Yuko peke yake kwenye baraste akijikokota kwa mwendo wa kobe huku fimbo iliofumbatwa katikati ya mikono yake ikimuelekeza njia. Kwa bahati mbaya, kipofu yule anajikwaa na jiwe lilompelekea  kupoteza ukucha wa mguu wake na kumuacha na kidonda. Je? kipofu yule atatumia njia ile anapotaka kwenda mkahawani tena? Abadan Katan.  Funzo alilopata kwenye mkasa ule halitamruhusu atumie njia ile kwa mara ya pili kwasababu ya hofu. Badala yake, atajizatiti kutafuta njia mbadala itakayomfikisha mkahawani. Hivyo ndivyo  elimu inapaswa kufunzwa kutoka shule ya chekechea  hadi chuo kikuu.

Mfumo wa elimu wa kisasa umedekeza wanafunzi wengi kwa kuweka pazia kwenye macho yao na kuwafanya washindwe kuona uhalisia wa maisha. Ukiwadadisi kwa undani wakwasi waliofanikiwa kimaisha, utakuta ya kwamba ufunguo wa mafanikio yao si elimu ya vitabu bali ni elimu ya maisha. Walikumbana ana kwa ana na uhalisia wa maisha wakiwa mashababi. Aidha, walijikuna walipowashwa kwani kupata mtu wa kuwakuna ilikua sawia na kusubiri boribo chini ya mnazi. 

 Itachukua zaidi ya miongo miwili kwa ‘wasomi’ kuelewa uhalisia wa maisha. Hata baada ya kupata shahada, wengi bado hawana ujuzi wa kufungua ukurusa wao mpya  wa maisha. Kwanini? Tangu chekechea, elimu inayofunzwa haiambatani na masaibu yoyote yanayompa mwanafunzi motisha ya kuendelea kupokea elimu . Wanafunzi wangekumbana vipi na uhalisia wa maisha ilhali wanasoma kwenye madarasa yaliyobuniwa na starehe ainati wakiwa na uhakika wa kupata chamcha bila bughdha. Wengi hawakupatwa na changamoto zilizowafanya kutafakari kuhusu msimamo wao kimaisha. Hawakua na motisha iliyowafanya kwenda shule. Wengi walienda shule kwasababu ni mazoea kwa kila mtu kwenda shule. Kitafutwacho shuleni hakijulikani. Ndiposa, hata baada  ya kukamilisha elimu ya chuo kikuu, wengi wamekuwa juha-kalulu katika maisha, hawajui pa kuanzia.

Kando na ‘wasomi’, wako ambao hawajabrikiwa kutua miguu yao kwenye lango la shule wala hawajapata kushuhudia maajabu ya kalamu kucharaza wino kwenye karatasi zilizojumlishwa na jalada kutengeneza kitabu.  Elimu wanayoisoma ni ya maisha, walimu ni hali duni ya maisha wanayoipitia na mitihani ni changamoto zinazowakumba. Abadan, hakuna mafanikio makubwa kama kupasi mtihani wa kimaisha. Chambilecho tunawaona mabwenyenye kama kina Bill Gates. Baada ya kujikwaa mara kadhaa wakitafuta njia sahihi ya kuwafikisha walikotamani kufika, njiani walijifunza mengi yaliyowapelekea hatimaye kupata njia iliyofungua milango ya mafanikio yao.

Elimu ya shuleni ingekamilika iwapo maarifa yangejumuishwa kwenye silabasi. Bila ya hivyo, jinamizi la ukosefu wa ajira halitamalizika karibuni. Ndio maana hakuna tofauti kubwa kati ya profesa na mwendawazimu ama mwerevu na mjinga. Wikendi njema waungwana.

Mwandishi: Ramadhan O. Sigomba

Baruapepe: omarramadhan163@gmail.com

Twitter: @RamadhanOmar17

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s