THITIMA NAKULIAA!

BY EVANS MAKOKHA

Chakula nianzapo kupika.

haraka mbio wajiondoa,

sikitiko moyoni labakia,

lawama mwelekezee mkubwa,

thitima nakuliaa!

Soweto mekuwa taabani,

waadhiriwa wengi ni sisi,

mtambo umeme hutengezeki,

tangu jadi mekuwa ahadi

thitima nakuliaa!

Nianzapo zangu kubukua,

kupitia yale mefunzwa,

giza totoro laingia,

hakika kusoma nashindwa,

thitima nakuliaa!

Ubinadamu nao tudumishe,

upoteapo dhamani umeme,

uhayawani nao tuuambe,

kistaarabu piga kelele,

thitima nakuliaa!

Menihadaa mengi kaski,

marekebisho yamo njiani,

matokeo yake siyaoni,

giza lanisakama machoni,

thitima nakuliaa!

Yangu tamati nimeshafika,

changu kilio kimesikika,

Bwana chansella tenda,

shukurani nazo tutakupa,

thitima nakuliaa!

 

The writer is a first year journalism student

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s